Zinazobamba

Samatta kamshangaza kocha Dean Smith baada ya kukaa mwezi

Kocha wa club ya Aston Villa Dean Smith amemwagia sifa na kumpongeza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anayekipiga Aston Villa ya England kuwa mchezaji huyo ni mpambanaji na amekuwa akiimarika zaidi kwa haraka ndani ya mwezi mmoja.
“Amewashangaza wachezaji wetu wengi sana kutokana namna ya ubora wake alivyo, ana movement nzuri na anaelewa mchezo, anaweza kuungana na timu mapema sana pia amefunga goli lake la kwanza la Ligi Kuu anaweza kuwa asset”>>>Dean Smith
Dean Smith ametoa kauli hiyo Aston Villa wakiwa wanaelekea kucheza dhidi ya Southampton katika mchezo wa EPL, Samatta akiwa anatoka kucheza dhidi ya Tottenham Hotspurs na kutoa presha iliyotoa goli la kwanza la Aston Villa kwa beki wa Tottenham kujifunga.

Hakuna maoni