VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUWASILISHA KWA WAKATI TAARIFA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI WA 2025.
Na Mussa Augustine
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Mohamed Ally Ahmed amevitaka Vyama vya siasa Nchini kuwasilisha kwa wakati taarifa za gharama ya uchaguzi Mkuu wa 2025.
Ametoa agizo hilo leo Machi 10,2026 jijini Dar es salaam wakati akifungua warsha ya siku moja kwa Viongozi wa Vyama vya saisa kwa ajili ya kupata elimu juu ya sheria ya gharama za uchaguzi ambayo inavitaka vyama hivyo kubainisha kiasi cha fedha kitakachotumika kabla na baada ya uchaguzi.
"Kama mnavyofahamu tumekua na sheria zetu za uchaguzi ambazo zinasimamia masuala mazima ya Vyama katika kuonesha Vyama kabla na baada ya uchaguzi na taratibu ambazo mnatakiwa mzifuate katika sheria hizo,baadhi ya sheria hizo ni sheria ya gharama ya chaguzi"amesema
Nakuongeza "leo tumekutana hapa kwa lengo la kujadili sheria ya gharama za uchaguzi,sheria hii kwa kawaida inavitaka vyama vya siasa,wagombea kujaza fomu za gharama za uchaguzi ambazo zitakua zinaonesha matumizi yao ya fedha zitakazotumika kabla na baada ya uchaguzi,pia wagombea wanapswa kujaza fomu kuelezea namna gani wametumia fedha hizo na wapi walizipata fedha hizo.
Aidha amesema kuwa kwa kufanya hivyo inasaidia kulinda Demokrasia kwa kutoa vyanzo halali vya fedha ndani ya nchi nakuepuka fedha zinazotoka nje ya nchi nakuleta ushawishi mmbaya,pia kuepuka fedha haramu zisitumike nchini nakuleta taswira mbaya kwenye Vyama vya saisa.
Amesema kuwa hatua hiyo pia inasaidia kuweka ukomo wa Vyama ambavyo havina fedha visizidiwe kupitiliza na Vyama ambavyo vina fedha,pamoja na Vyama vyenye uwezo wa kifedha visitumie fedha nyingi kupitiliza hadi kupoka demokrasia.
"Sheria ya gharama ya uchaguzi imeweka usawa angalau alie nacho na asie nacho kushiriki uchaguzi katika demokrasia ya nchi hii"amesem
Kwa upande wake mwenyekiti baraza la Vyama vya siasa Nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ADA TADEA Juma Ali Khatib amesema kuwa zimesalia siku 112 kufikia tarehe 26 Juni,ambao ndio mwezi wa mwisho wa kuwasilisha fomu za taarifa ya gharama za uchaguzi hivyo amevitaka Vyama vya saisa kutumia muda huo ipasavyo ili kutekeza takwa la kisheria.
Kwa upande wake mwenyekiti baraza la Vyama vya siasa Nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ADA TADEA Juma Ali Khatib amesema kuwa zimesalia siku 112 kufikia tarehe 26 Juni,ambao ndio mwezi wa mwisho wa kuwasilisha fomu za taarifa ya gharama za uchaguzi hivyo amevitaka Vyama vya saisa kutumia muda huo ipasavyo ili kutekeza takwa la kisheria."Siku hizi zilizobaki bado mpo ndani ya muda kuhakikisha mnajaza fomu na kuziwasilisha,kama kuna changamoto yoyote basi tutashirikiana kuelezana kupitia warsha hii,"amesema Khatib.
Nae Katibu Mkuu Taifa wa Chama Cha NLD ambaye pia alikua mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Doyo Hassan Doyo ameishukuru ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa kwa kuandaa warsha hiyo nakusisitiza kuwa itasaidia kuongeza uelewa kuhusua sheria za uchaguzi ikiwemo sheria ya gharama za uchaguzi.
"Kinachotakiwa sasa hivi ni kujaza fomu kwa ajili ya kuonesha mgombea Urais ametumia kiasi gani cha fedha,na zimetoka wapi,na vyanzo vyake,hivyo lazima kua na uelewa wa kutosha kufanya kazi hiyo vizuri,sisi kama Viongozi wa Vyama vya siasa kwa kupata mafunzo haya ya kujaza fomu tumepokea kwa furaha kubwa".amesema Doyo
Halikadhalika Naibu Katibu Mkuu wa Act Wazalendo Bi.Ester Thomas amesema kuwa sheria ya gharama ya uchaguzi ni muhimu ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma kulikua na ubadhilifu wa fedha
wakati wa uchaguzi.
"Hili ni jambo kubwa sana hasa kwa akipindi hiki ambacho sisi wote tunafahamu kumekua na ubadhilifu mkubwa sana wa fedha katika kipindi cha uchaguzi,na ndio maana sheria hii imekuja na nimara ya pili inatumika yaani 2020 na 2025,kubwa zaidi sheria hii inaweka usawa wa matumizi ya fedha kwa Vyama vya saisa."amesema.



No comments
Post a Comment