Zinazobamba

Wanne wakamatwa kwa kuweka sauti za milipuko kwenye bodaboda.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dare es Salaam limewakamata watu wanne  na pikipiki zao, kwa tuhuma za kusababisha kero na fujo kwenye makazi ya watu kutokana na kuweka sauti za milipuko kwenye vyombo vyao vya moto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo kwa vyombo vya habari,milipuko hiyo husababisha kero kwa wananchi jambo ambalo ni kosa na kinyume cha Sheria ya Usalama Barabarani.

Watuhumiwa hao wanne wametajwa  kuwa ni Abdallah Masumbuko mkazi wa Tabata, Julius Dismas, mkazi wa Mwananyamala, Salehe Ally, mkazi wa Kijitonyama, Mohamed Rashid mkazi

wa Magomeni, ambao wote wapo mahabusu na hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria.

Hata hivyo jeshi hilo linatoa wito kwa watumiaji wote wa barabara wakiwemo waendesha vyombo vya moto kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani pasipo kubugudhi watumiaji wengine na wananchi Kwa jumla.

No comments