Zinazobamba

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAKINI WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA CCM.


Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Makini Mh.Coaster Jimmy Kibonde ametoa rai kwa wanachama wa Chama kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani katika kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyika.

Rai hiyo ameitoa leo Machi 5,2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa Serikali iliyopo madarakani niya Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo wanachama wa Makini hawana budi kushirikiana nayo.

Aidha Mh.Kibonde ambaye pia alikua mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025 amesema kuwa uchaguzi mkuu umepita na sasa kilichobaki ni Chama kilichoshika dola kitekeleze ahadi zote kilichoahidi kwa Wananchi wakati wa kampeni kwani kikifanya hivyo kitakua kimeleta maendeleo kwa Watanzania wote.

"Kila Chama kilichoshiriki kwenye uchaguzi Mkuu wa 2025 kilikua na Ilani nzuri,lakini mnapokua kwenye ushindani lazima mshindi apatikane mmoja,hivyo CCM ilishinda,tunaomba sana Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Dkt.Samia itekeleze ahadi zake kwa Wananchi."amesema

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo machachari wa kisiasa amewasihi vijana maarufu kama Gen-z kukataa kutumika kwa uvunjifu wa amani Nchini.

"Niwasihi sana vijana wasirubuniwe na watu wasiolitakia amani Taifa letu,serikali imeanzisha wizara mahususi kwa ajili ya kushughulikia mambo yanayowahusu vijana hivyo wawe watulivu na wachangamkie fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali yao" amesema 

Pia Mh.Kibonde amewaomba baadhi ya Viongizi wa dini ambao wamekua sehemu ya uchochezi wa vurugu za uvunjifu wa amani kuacha tabia hiyo na badala yake watoe mahubiri yatakayo waleta pamoja watanzania nakuondoa hali ya kubaguana kidini.

"Hawa Viongozi wa dini wanaojiingiza kwenye siasa wananfanya kosa kubwa sana,wanachochea hali ya vurugu na uvunjifu wa amani kwenye Taifa letu,mimi nawaomba waache,wao wana wafuasi wengi sana hivyo wahubiri amani kwenye Taifa letu." amesema

Nakuongeza kuwa"nawaomba wananchi kuendelea kulinda amani,utulivu na mshikamano kwani tunu hizi zikipotea hakuna mtanzania yeyote ambaye ataweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na Kijamii.



No comments