Zinazobamba

TAKUKURU TEMEKE YAMFIKISHA ASKOFU NYALALI MAHAKAMANI.


*Nikutokana na tuhuma za kughushi nyaraka ili kujipatia kiwanja chenye thamani ya shilingi milioni 60.

Na Mussa Augustine.

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Temeke imemfikisha mahakamani Askofu Renatus Joseph Nyalali wa kanisa la Hosanna Assemblies of God Tanzania(HAOGT)kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kutoa nyaraka za uongo zinazohusiana na umiliki wa ardhi ili awze kujipatia kiwanja chenye thamani ya shilingi millioni 60.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mach 5 ,2026 na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Temeke Ismail Bukuku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2025.

Bukuku amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na TAKUKURU baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mmoja wa warithi na msimamizi wa mirathi ya marehemu Ally Hamad Hillal.

Aidha amesema kuwa kutokana na ushahidi uliokusanywa na kufanyiwa uchambuzi wa kitaalamu TAKUKURU imefungua kesi ya jinai namba CC/26097/2025 dhidi ya Askofu huyo katika mahakama ya wilaya ya Kigamboni.

"Kwa mujibu wa hati ya mashtaka imedaiwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022,mshtakiwa alighushi nyaraka na sahihi za wanafamilia wa marehemu kwa lengo la kujipatia umiliki wa eneo la ardhi lililopo Mtaa wa Kizani Gezaulole Wilayani Kigamboni" amesema Bukuku 

Nakuongeza "Eneo hilo lilinunuliwa mwaka 2008 kwa kiasi cha shilingi milioni sitini na kuachwa kama urithi kwa watoto wa marehemu."

Kwa mujibu wa Bukuku amesema Mshtakiwa alitumia mwanya wa kuaminiwa na familia ya marehemu kuandaa nyaraka za uwakilishi ( Power of Attorney)kwa njia isiyo halali.

Aidha amesema nyaraka hizo zilitumika kupima eneo hilo na kuligawa katika viwanja tisa ambavyo baadaye vilikuwa vikiuzwa kwa watu mbalimbali kwa kutumia majina na sahihi za kughushi za wanafamilia nakwamba uchunguzi umebaini kuwa katika baadhi ya viwanja hivyo mtuhumiwa alijiorodhesha mwenyewe kama mmiliki halali.

"TAKUKURU inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na itaendelea kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vyote vya rushwa,udanganyifu na uhalifu wa aina yoyote bila kuzingatia hadhi ya mhusika kwa lengo la kulinda maslahi ya umma na misingi ya haki " amesema 

No comments