JUKWAA LA GONGA KENGELE KWA USAWA WA JINSIA LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

*Lazitaka kampuni binafsi kuzingatia usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi.
Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Compact Tanzania Marsha Macatta-Yambi ametoa rai kwa makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuhakikisha zinakua na usawa wa kinjisia kuanzia nafasi za juu za uongozi.
Bi.Marsha Macatta-Yambi ambaye pia Kiongozi wa umoja wa wandaaji wa jukwaa la Gonga kengele kwa usawa wa jinsia (Ring the bell for gander Quality)amesema hayo leo March 6,2026 jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani inayotarajiwa kufanyika March 8 mwaka huu.
Aidha amesema kwamba jukwaa la gonga kengele kwa usawa wa jinsia (Ring the bell for gander Quality) ni kukumbusha masuala mazima ya usawa wa kinjisia katika jamii.
"Kwetu sisi tunaleta jukwaa(Platform) hii kuhakikisha kwamba makampuni ya binafsi ambayo yapo Nchini Tanzania yanaingia kwenye utaratibu wa kuhakikisha yanaweka usawa wa kijinzsia"amesema
Nakuongeza,"kwanza kwa kuhakikisha wanavyoingia hua sio kitu cha mmoja mmoja bali uongozi wote pamoja na bodi,pia kuhakikisha wanajitathmini kwa sera(Policy) na mikakati ya kwenda kwa pamoja katika usawa wa kijinsia bila kupendelea jinsia yoyote.
Amesema kuwa Viongozi wa makampuni au Taasisi wanatakiwa kujitathmini wao wenyewe nakuachana na masuala ya kung'ang'ania takwimu(Data),nakwamba mara nyingi oganaizesheni zinaingia lakini hazijitathmini nakuangalia mapungufu ya aina gani yaliyopo kwa wafanyakazi wao na kuhakikisha wanalenga uwepo wa usawa wa jinsia.
Amesema kuwa katika jukwaa hilo (platform)wanahakikisha wanawapa misingi ya kufanyia kazi na wanahakikisha kwamba wanazichukua na kuzifanyia kazi takwimu walizonazo na kutengeneza mpango wa kuingiza kwenye mipango yao ya kila siku.
"Makampuni yanakosa viwango hali ambayo inapekekea wafanyakazi kuacha kazi,vilevile kushiriki kwa ila mtumishi mmoja mmoja hupungua nakua kiwango cha chini nakuifanya kampuni ipate mavuno kidogo tofauti na matarajio yake."amesema
Vilevile amebainisha kwamba mwaka huu 2026 Tanzania itatoa ripoti ya tatu katika kuona ni jinsi gani tumeendelea kutenda katika malengo yote ya maendeleo(SDG'S),hatua itasaidia kugundua mwelekeo wa dira ya maendeleo ya 2050,nakupitia ripoti hiyo itaonesha maeneo yaliyofanyika kwa upana.
No comments
Post a Comment