Rais Magufuli Amwaga Ajira 1000 Kwa Madaktari...."Tuanze na madaktari 1000, mambo yakiwa vizuri tena tutaajiri wengine"
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ametoa
kibali kwa Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora inayoongozwa na Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika kuajiri
madaktari 1000.
Rais
Magufuli ametoa kibali hicho jana alpohudhuria maadhimisho ya siku ya
madaktari katika ukumbi wa mikutanao wa kimataifa wa Julius Nyerere.
“Ninafahamu kuna madaktari 2700 bado hawajaajiriwa, nitalifanyia kazi” alisema Rais Magufuli na kuendelea kwa kumuuliza Waziri Mkuchika uwezekano wa kuajiri Madaktari 1000.
“Tuajiri madaktari 1000 na wasambazwe vizuri katika Mikoa yote” alisema Rasi Magufuli kauli ambayo ilipokelewa kwa furaha na shangwe kutoka kwa wajumbe waliohudhuria Mkutano huo wa 55 wa Chama cha madaktari Tanzania (MAT)

Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza nguvu kubwa
kwenye Sekta ya Afya nchini kwa kujenga miundombinu (majengo) pamoja na
ununuzi wa vifaatiba na mashine za kitaalam na kusema kuwa bila ya kuwa
na wataalam wa kutosha bado Sekta ya Afya itakabiliwa na changamoto za
upatikanaji wa huduma bora za afya.
“Tuanze na madaktari 1000, mambo yakiwa vizuri tena tutaajiri wengine, tunahitaji madaktari mpaka vijijni, tumejenga vituo vya afya 352 tumejenga Hospitali za Wilaya 77 zote hizi zinahitaji madaktari” alisema Rais Magufuli.

Magufuli ameonyeshwa kufurahishwa na utendaji kazi wa madaktari ambao
wanatumia muda mwingi kuokoa maisha ya watanzania na kuwaahidi
kuzishughulikia changamoto walizonazo ili waweze kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni