NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA AWATAKA WATUMISHI NIDA KUTUNZA SIRI, KUSHIRIKIANA NA KUWAJIBIKA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(katikati) akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la
Wafanyakazi, Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kailima aliwataka watumishi wa
NIDA kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji kwa upande wa mwajiri
na mwajiriwa, pamoja na kutunza siri za ofisi. Kulia ni Mwenyekiti wa
Baraza hilo, Dkt. Arnold Kihaule. Kushoto ni Katibu wa Baraza, Lulu
Ishengoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(wapili kushoto meza kuu), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule (wapili
kulia meza kuu), Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Hassa Hassan (kulia),
Katibu wa Baraza hilo, Lulu Ishengoma (kushoto), wakiimba wimbo wa
mshikamano wakati wa Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika jijini Dar es
Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule akizungumza katika Kikao cha Baraza
hilo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Mgeni rasmi wa Kikao
hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani
Kailima (wapili kushoto) aliwataka watumishi wa NIDA kufanya kazi kwa
kushirikiana, uwajibikaji kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa, pamoja na
kutunza siri za ofisi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hassan
Hassan. Na kushoto ni Katibu wa Baraza, Lulu Ishengoma. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati
alipokuwa anawasili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufungua
kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (katikati) akizungumza wakati akifungua
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Tawi la Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kailima
aliwataka watumishi wa NIDA kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji
kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa, pamoja na kutunza siri za ofisi.
Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Arnold Kihaule. Na kushoto ni
Katibu wa Baraza, Lulu Ishengoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Na Felix Mwagara, MOHA.
NAIBU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima
amewataka watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya
kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji na kutunza siri za ofisi kwa mujibu
wa sheria.
Akizungumza
wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Tawi la NIDA, Kailima
alisema mafanikio ya Mamlaka hiyo ni pamoja na kushirikiana katika
utendaji wa kazi ili kuleta weledi, na pia kuepuka kutoa siri za ofisi
kwa mujibu wa utaratibu wa utumishi wa umma.
Pia
aliwakumbusha watumishi hao kutoka Makao Makuu ya NIDA na Ofisi zake
Mikoani, kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo kwa upande wa mwajiri na
mwajiriwa kwa kufanyiwa kazi kile kinachotakiwa kufanyiwa kazi na
kisichohitajika kuifanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.
“Tukoseane
kwa nia ya kuboresha, tusikoseane kwa nia ya kubomoa kwa sababu ya
kupata fursa hii ya kuwa na haki na hadhi sawa, na pande zote mbili
ziwajibike kuwajibishana,” alisema Kailima.
Aliongeza
kuwa, watumishi wanapaswa kupewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za
mamlaka na masuala yanayowahusu kwa utaratibu wa ofisi au unaoidhinishwa
na Mkurugenzi Mkuu na si vinginevyo.
“Muhakikishe
mnatoa huduma kwa wananchi sehemu zote nchini kwa weledi, maafisa
wafike mapema katika maeneo ya kazi na kutoa vitambulisho vya Taifa
mapema, na wananchi waridhike na huduma hiyo mnayoitoa, kwa hatua hiyo
mtapunguza malalamiko ya wananchi,” alisema Kailima.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka hiyo, Dkt. Arnold Kihaule alitoa mafanikio ya Mamlaka yake hadi
kufikia Desemba mwaka 2019, alisema NIDA imefanikiwa kusajili wananchi
21,511,321, Wageni wakaazi, 19,311 na Wakimbizi 274,000 kutoka Tanzania
Bara na Zanzibar.
“Pia
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imezalisha namba za utambulisho
16,211,654 na kutoa vitambulisho 5,787,869, na vimewafikia wananchi
ilipofika mwezi Desemba 2019,” alisema Dkt. Kihaule.
Kikao
cha Baraza hilo cha siku moja pia kilipitia Utekelezaji wa Bajeti ya
Mwaka 2019/20 kwa Kipindi cha kwanza cha Mwezi Julai hadi Desemba na
Makadirio ya Bajeti ya Mamlaka kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni