TAMWA WAAZIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE KWA KUWAOMBA SERIKALI, WAZAZI KUDHIBITI VYANZO VYA MIMBA ZA UTOTONI
Afisa mipango (strategic manager) Bw. Davis Lumala (mwenye koti la blue) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Edda Sanga. |
Mmoja wa waandishi wa habari akizungumza katika mkutano huo. |
Na Magali:
CHAMA cha wandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa upatikanaji wa pedi bure kwenye shule ili kumfanya mtoto wa kike awe na mazingira mazuri na rafiki anapokuwa darasani.
Akizungumza na wandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Kike, yenye kaulimbiu Tokomeza mimba za utotoni tufikie Uchumi wa viwanda, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga, alisema wasichana wengi huishia kurubuniwa na kununuliwa na wanaume kwa kukosa fedha za kununulia vifaa hivyo wakibeba mimba huwatelekezwa.
"Ni jukumu la wazazi pamoja na jamii nzima kwa ujumla kutoa elimu ya kijinsia kwa watoto wa kike ili waweze kujitambua na hatimaye kuwezesha kuhimili vishawishi ambavyo husababisha kupata mimba katika umri mdogo," alisema Edda.
Alisema Serikali inayowajibu wa kuwajengea wanafunzi mabweni karibu na shule ili kuondoa changamoto wanazokumbana nazo njiani pindi wanaporudi majumbani kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia watoto kupata mazingira rafiki kwa ajili ya kujisomea na kutimiza malengo yao.
Mkurugenzi alisema Takwimu za Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinaonesha kuwa wasichana 36 kati ya 100 huolewa kabla ya wakati huku wengine 27 kati ya 100 ambapo mkoa wa Katavi ndio unaoongoza kuwa na mimba za utotoni kwa asilimi 45.
Aidha mikoa mingine inayokumbwa na tatizo hilo kuwa ni pamoja na Mkoa wa Tabora asilimia 43,
Dodoma asilimia 39, Mara asilimia 37, Shinyanga asilimia 34 na kifaifa tatizo hilo linaonesha ni kwa asilimia 2.
"Kuendelea kwa vitendo hivyo ni kukiuka haki za mtoto ambapo inatutaka kwa pamoja tumlinde mtoto wa kike na pia tuweke mikakati ya kuzuia ukatili huo hivyo kuna umuhimu wa kushirikiana na wadau na asasi mbalimbali za kiraia ili kutokomeza ndoa za utotoni japo changamoto mojawapo ni ile ya sheria ya ndoa.
"Sheria hiyo iliyopo inamruhusu mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 aolewe kwa idhini ya wazazi au walezi ambapo familia nyingi hufanya hivyo kutokana na hali ngumu ya kimaisha ili wapate fedha zitokanazo na mahari wanazopewa," alisema.