Zinazobamba

BREAKING NEWS,POLISI WENYE SILAHA WAVAMIA MKUTANO WA SHEIKH PONDA NA WAANDISHI WA HABARI,SOMA HAPO KUJUA


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida  watu wanaodhaniwa kuwa Polisi,wamevamia mkutano wa waandishi uliohitishwa na  Katibu Mkuu Jumuiya na Taasisi za Kislam nchini,Sheikh Ponda Issa Ponda na kufanikiwa kuondoka na waandishi Wa Habari.Anaandika KAROLI VISENT endelea nayo

Sheikh Ponda ambaye alihitisha mkutano na waandishi uliofanyika kwenye Hotel ya IRIS iliopo mtaa Wa Amani Kariakoo Jijini Dar es Salaam..

Katika mkutano huo waandishi wa Habari walifika  ambapo  Sheikh Ponda alikuwa anazungumza na waandishi hao ,Kuhusu safari yake aliyokwenda Nairobi nchini Kenya alipolazwa Mbunge Wa Singida Masharki Tundu Lissu kutokana kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma mwezi uliopita.

Katika mkutano huo Ponda alivitumu vyombo vya dola kwa kushindwa kuzuia vitendo vya uhalifu ikiwemo matukio ya kutekwa,kupigwa risasi kwa wanasiasa pamoja kukamatwa hovyo viongozi wa dini ya kiislam nchini.

SEKESEKE LA KUVAMIWA LILIVYOKUWA.

Mara baada ya Sheikh Ponda kumaliza kuongea na wanahabari hao ,sheikh huyo na wenzake walikuwa wanashughulikia taratibu za kuwapatia wanahabari hao ikiwemo Hutuba yake pamoja na taratibu zingine.

Sheikh Ponda na wenzake hao walitoka kwenye ukumbi waliokuwepo wanahabari na kuingia  kwenye Chumba kinachofuata kwa ajili ya kuwapatia waandishi taratibu hizo.

Wakati Sheikh Ponda alipotoka Ghafla wakatokea watu waliovalia nguo za kiraia huku wakiwa na simu ya upepo(Redio Call) wakaingia moja kwa moja kwenye ukumbi waliopo waandishi wa Habari na kumuulizia Sheikh Ponda alipo.

Waaandishi waliposema Sheikh Ponda yupo kwenye chumba kinachofuata , Polisi  hao wakaenda kwenye chumba hicho na kumkuta Sheikh huyo ameondoka .

Baada ya Polisi kumkuta hayupo ,wakawafuata waaandishi wa Habari ambapo wakasema "Hakuna mwandishi wa Habari humu  kutoka mpaka Sheikh Ponda aonekane" ilisikika Kauli hiyo kutoka kwa mmoja wa askari hao.

Polisi hao wakamfuata Meneja wa Hoteli na kuanza kufanya ukaguzi kwenye Chumba hadi Chumba  katika Hoteli kumsaka kiongozi huyo wa Kiroho alipo.

Baada ya kufanya msako huo, Polisi hawakufanikiwa kumkamata kutokana na Sheikh Ponda kuwazidi Ujanja Polisi baada ya kuwatoroka.

Polisi hao wakawafuata tena, Waaandishi wa Habari waliowazuia na kumwamulu mwandishi wa TV ya Online, Ahmed Kombo na kumtaka waaende naye ili akawape mkanda wa video aliyemrekodi Sheikh Ponda.huku pia  wakaruhusu waaandishi wengine waondoke eneo hilo.

NJE YA HOTELI ILIVYOKUWA.

Mwandishi wa Fullhabari.Blog ambaye alikuwa ni miongoni mwa waaandishi hao wa Habari alishudia Gari mbili  za Polisi aina ya Difenda pamoja na askari kwenye silaha wakiwa wamezingila Hoteli huyo .

Wakati Polisi wakiwa wanatoka nje ya Hoteli huyo,Mwandishi na Mpiga Picha  wa Gazeti la Nipashe, John Badi ambaye alikuwa akiwapiga picha askari hao akajikuta naye akamatwa na kuondoka nao