Zinazobamba

DR.MAGEMBE AWAONYA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,VIJIJI NA VITONGOJI.

Dr.Grace Magembe

Dr. Grace Magembe akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa serikali za Mitaa, Mwenyekiti wa JUMIKITA Shaaban Matwebe

Na Mussa Augustine.

Naibu Katibu Mkuu OR -TAMISEMI  Dr. Grace Magembe ametoa maelekezo kwa Waandishi wa habari za mitandaoni kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao katika kuripoti uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 ,2024.

Dr.Magembe ametoa maelekezo hayo leo Novemba 13,2024 wakati akifungua semina ya Waandishi wa habari za mitandaoni iliyoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa habari za mitandaoni(JUMIKITA)ikiwa lengo ni kuwafundiaha kanuni za uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Aidha amesema kuwa Waandishi wa habari wanapaswa kutoa taarifa za uelewa mpana kwa wananchi ili wajue umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi pamoja na kupima sera na maono ya wagombea wa nafasi hizo katika kuwaletea Maendeleo wananchi wa eneo husika.

"Naomba niwasisitize mambo kadhaa ikiwemo kuandika habari zinazosimamia misingi ya haki na usawa kwa wagombea wote ili kuleta utulivu na amani nchini" amesema Dr.Magembe

Nakuongeza kuwa,"Epukeni kuripoti habari za taharuki kwenye nchi,msisababishe uvunjifu wa amani,epukeni taarifa za kuwatenganisha Watanzania bali mripoti habari zenye kuleta mshikamano na upendo katika kipindi hiki cha uchaguzi" amesisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa TAMISEMI

Hata ivyo ametoa maelekezo kwa mamlaka zinazosimamia uchaguzi huo kuhakikisha zinatenga maeneo mazuri yenye utulivu ambayo yatatumiwa na Waandishi wa habari wakati wakitimiza majukumu yao  ya kuripoti uchaguzi huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shaaban Matwebe amewasihi Waandishi wa habari za mitandaoni kushirikiana na Serikali kupitia TAMISEMI katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji  kwa ajili ya kuhabarisha jamii kushiriki uchaguzi huo kwa amani.

"Naomba sana ndugu zangu Wanahabari nyinyi ni Jeshi kubwa ,naomba tushirikiane na TAMISEMI katika zoezi hili lenye sura ya Kitaifa tuwe Wazalendo turipoti habari hizi kwa nguvu zetu zote ili tutoe uelewa mpana kwa wananchi  kuhusu uchaguzi huu wa serikali za mitaa." amesema Matweve

Baadhi ya Waandishi wa habari walioshiriki semina hiyo wamesema kuwa wapo tayari kushirikiana na TAMISEMI katika kipindi hiki Cha uchaguzi ili kuhakikisha tunu za Taifa kama vile amani,utilivu na mshikamano zinalindwa.


Hakuna maoni