MILA POTOFU ZACHANGIA WANAWAKE KUBAGULIWA KWENYE SHUGHULI ZA MADINI
Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili Bw,Clarence Kipobota,akiwakilisha taarifa ya awali ya utafiti ya ujumuishwaji wa masuala ya jinsia katika sekta ya madini Mkoani Geita. |
Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya madini Mkoani Geita. |
Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili Bw,Clarence Kipobota,akielezea vitendo vya mira potofu ambavyo vimekuwa vikiwakandamiza wanawake kwenye maeneo ya machimbo ya dhahabu. |
Afisa Mradi wa BHRT Theresia Sawaya akizungumzia shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na shirika hilo. |
Wadau wa Taasisi mbali mbali wakifuatilia maelezo ya afisa Mradi wa BHRT. |
Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la
biashara na haki za binadamu (BHRT) limebaini
kwenye sekta ya madini bado kuna mila
potofu zinazomkandamiza
mwanamke kushiriki kwenye sekta ya madini kutokna na kwamba mwanamke
akishiriki kwenye uchimbaji wa madini akiwa kwenye mzunguko wake wa mwezi ni
mkosi na anaweza kusababisha madini kutopatikana pindi anapokuwa kwenye kipindi
hicho.
Akizungumza
kwenye Mkutano ambao umewakutanisha wananchi wa Mkoani Geita na baadhi ya
taasisi ,Mtafiti mkuu wa mradi wa BHRT , Wakili bw Clarence Kipobota,amesema
kuwa wakati wanafanya utafiti wamebaini kuwa kundi la wanawake ni watu ambao wamekuwa
wakikandamizwa kwa kiasi kikubwa kwenye shughuli za madini kutokana na kuwepo
kwa mila potifu na mfumo dume.
“Tumebaini
kuwa kuna swala la mila potofu kwamba mwanamke anapokuwa kwenye siku zake
haruhusiwi kwenda mlimani kufanya shughuli za uchimbaji kutokana na kwamba
anaweza kusababisha madini kutokupatikana”Alisema Kipoboto.
Aidha kwa
upande wake Bi,Christina Gamba ameelezea kuwa
wanawake wamekuwa wakipata manyanyaso ya kuzuiliwa kwenda mlimani kuchimba madini kutokana na kuwepo kwa mila
potofu kuwa mwanamke akienda maeneo ya uchimbaji ni Mkosi na mwisho wa siku
huishia kufanya shughuli za uchenjuaji.
Katibu
Mtendaji wa shirika la maendeleo ya vijana ,Bw Makanya Tumbo amesisitiza
kuendelea kuwekwa sawa kwa takwimu za ushirikishwaji wa maswala ya Kijisia .
Afisa Mradi
Theresia Sawaya ameelezea lengo la shirikia hilo ni kuendelea kufanya utetezi
wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuangalia swala zima la ukiukwaji wa
haki za Binadamu ili kuleta utetezi wa
Binadamu.