PIKIPIKI ZA KINGLION ZINAVYOTATUA TATIZO LA USAFIRI VIJIJINI
Na Magali
Afisa Mtendaji msaidizi wa Kampuni hiyo, Bw Arnold Lymo maarufu kama (Riziki) akionyesha baadhi ya pikipiki ambazo zinafanya vizuri huko vijijini |
Ukizungumzia
pikipiki zinazofanya vizuri katika soko
Tanzania, huwezikukosa kutaja pikipiki
za Kinglion, ni pikipiki ambazo katika kipindi kifupi zimeweza kuteka soko la
vijijini na kutatua kabisa kero ambazo kwa hakika zilikuwa changamoto.
Iko
hivi, pikipiki za Kinglion kwa sasa ndiyo zimeshika soko la Tanzania, ni
pikipiki ambazo zimeanza kama “underdog” yaani siyo tishio lakini taratibu
watanzania wameanza kuziamini na kuzimia kuliko pikipiki zingine zozote kwa
sasa.
Huwezi
kubisha… utafiti uliofanywa na mtandao wa Fullhabari Blog unaonyesha Pikipiki
za Kinglion zimeweza kuenena kwa kasi ya kimbunga katika soko la Tanzania
hussani maeneo ya vijinini, Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakikimbilia
pikipiki za Kinglion, ni aghalabu sana
kuzikuta pikipiki zingine maeneo ya vijijini…kila kona ya kijiji ni
Kinglion!Kinglion!Kinglion.
Kufuatia
hali hiyo…Fullhabari Blog ilimtafuta Afisa Mtendaji Msaidizi wa kampuni ya
Kinglion Investment Co. Ltd ili kufahamu “siri” ya mafanikio hayo.
Akizungumza
na Fullhabari. Blog Afisa Mtendaji msaidizi wa Kampuni hiyo, Bw Arnold Lymo
maarufu kama (Riziki) amesema siri kubwa ya kampuni yao kukua kwa kasi hapa
Tanzania ni kujitoa kwao kusaidia jamii ya Tanzania kwa kuuza bidhaa zao kwa
bei ambayo ni rafiki lakini pia kutoa huduma bora kwa kujibu mahitaji ya walaji.
Riziki
amesema walijaribu kuliangalia soko kwa karibu na kujua jamii ya vijijini
inasumbuka na matatizo ya usafiri…wananchi wanatumia muda mrefu kutembea ili
kupata huduma… wengine inawachukua muda mrefu kubeba mizgo yao kufika majumbani
kwao…tumeona hiyo ni fursa na kuamua kuja na muarobaini utakaotatua kero hizo.
Riziki
anasema baada ya kuziona fursa hizo tukawa tunaagiza bidhaa kulingana na
mahitaji ya Wateja wetu…
Amesema
kwa vijijini wateja wengi walikuwa wanahitaji pikipiki ambazo zinaweza kubeba
mizigo mizito na ambayo haiwezi kuharibika kwa haraka.
Kufuatia
hali hiyo Kampuni iliamua kujipanga na kuamua kuleta pikipiki kulingana na
mahitaji jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kukua kwetu kwa haraka hadi
kufikia kushika nafasi ya kwanza katika soko la Tanzania.
“Watu
wengi hawafahamu…Kampuni yetu ndiyo namba mona hapa nchini kwa sasa, lakini
watu watakutajia wengine sisi haitushi
tunachojua ni kwamba tunafanya vizuri sokoni” Alisema Riziki.
Aidha
akizungumzia mipango ya baadae…Riziki amesema wamejipanga kuhakikisha wanatoa
huduma iliyo bora na itakayotatua changamoto za watu hususani huko vijijini.
Kama
unavyoona tumekuja na bidhaa zingine mpya hapa katika maonesho….lengo letu ni
kuwaonyesha watu nini tunafanya kuhakikisha huduma zinazotolewa ni bora…tunawahakikishia
watanzania kuwa sisi tutaendelea kutoa huduma iliyo bora na ya kuaminika.
Kampuni
ya Kinglion Toka kuanzishwa kwake tayali imefikisha miaka 10, na imeweza kuenea
Nchi nzima na kwamba bidhaa zake zimendelea kuaminika na watanzania walio
wengi.