Zinazobamba

BARNABAS MAPANDE AENDELEA KUSHIKIRIA NAFASI YA UWENYEKITI WA CCM WILAYA YA CHATO

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambaye amechaguliwa kushika nyazifa hiyo kwa mala ya Pili Barnabas Mhoja Mapande akiwashukuru wajumbe wa Mkutano huo kwa kuweza kumchagua kwa mala nyingine tena kuendelea kukiongoza chama hicho ngazi ya Wilaya.

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu akiwaelezea wajumbe kuhusu swala la kuendelea kutimiza ilani ya chama cha mapinduzi(CCM).

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia uchaguzi.

Mbunge wa Jimbo la Busanda Lolesia Bukwimba akielezea mikakati ya kuendelea kupeleka maendeleo kwenye jimbo la Busanda.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita ambaye pia ni Mbunge Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na wajumbe wa Mkutano huo.

Wajumbe wakiendelea na kufuatilia Mkutano.

Ukumbi ukiwa umesheheni wajumbe wa Mkutano huo.

Msimamizi wa uchaguzi huo Joel Ramadhani Machanya  ambae pia ni Katibu msaidizi na Mhasibu wa CCM Wilaya ya Mbongwe  akitangaza matokeo ya uchaguzi.

Kaimu Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye alikuwa akisimamia uchaguzi Ahamed Mbaraka akikabidhi madaraka kwa mwenyekiti aliyechaguliwa.

PICHA NA JOEL MADUKA.




Barnabas Mhoja Mapande  ,amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Geita,kwa kupata kura754  na kuweka rekodi ya kukiongoza chama hicho wilayani humo kwa awamu pili  mfululizo .

Akitangaza matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa CCM wilayani humo  ,msimamizi wa uchaguzi huo Joel Ramadhani Machanya  ambae pia ni Katibu msaidizi na Mhasibu wa CCM Wilaya ya Mbongwe , amesema kura ambazi zilipigwa ni 1291 na ambazo ziliharibika ni 166 hivyo kura harari 1125.

 Amesema kuwa   ,Mapande  ameshinda dhidi ya wagombea wenzake  Alhaji Saidi Mganda Mahoma alipata kura 35 na Adoado Ntwane Kazihoba amepata kura 336.


Aidha Machanya ameendelea kutaja  nafasi za   wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu Taifa kutoka CCM wilaya, kuwa ni Leornad Kiganga Bugomola Kura 657 ,Herman Clement Kapufi kura 681 na Constatine Molandi Mtani Kura 777.

Awali mbunge wa jimbo la Geita  Mjini Constatine Kanyasu  ,amesema  kazi yake kubwa ni kuendelea  kusimamia ilani ya chama kwa kuwatumikia   wananchi wa jimbo  huku akielezea shughuli ambazo hadi sasa ameendelea kuzitekeleza likiwemo swala la kupeleka umeme kwenye maeneo ambayo yapo nje ya mji pamoja na kuboresha miundo mbinu ya Barabara kwa kiwango cha Lami na Molamu na kwamba atahakikisha anashirikiana na viongozi hao kujenga na kutengeneza misingi mipya ya CCM mpya ,ili kutimiza madhumuni na kusudi la  mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. John Magufuli .

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mbunge Joseph Kasheku(Msukuma)ameewataka madiwani wa halmashauri mbili ya mji na Wilaya ambao hivi karibuni waliandamana kuelekea mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa madai ya kiasi cha sh Dola Milioni 12, ambao bado hawajafika polisi kwenda kwa pamoja kwaajili ya kusikiliza kile ambacho wanatakiwa kwenda kukijibu huku akidai yupo tayari kuendelea kukamatwa na Jeshi la Polisi kwasababu ya masirahi ya wananchi.


Kwa upande wake Barnabas Mhoja Mapande  ,amewashukuru  wajumbe waliomchagua na ambao awakumchagua  na kuwataka  kuvunja makundi ili kuendelea kukijenga chama hicho  .

Alisema kuwa  wajibu wa chama hicho ni kusimamia serikali na kwamba wajibu wa serikali ni kuendelea kuhimiza utekelezaji wa ilani ya chama hicho na wajibu wa mtumishi wa serikali ni kujua chama kinataka nini hivyo kama kuna mtendaji na mtumishi ambaye anakwenda kinyume na utekelezaji wa majukumu ni vyema wakakaa nao na kushughulika nao.

Pia amewataka wagombea ambao alikuwa akigombea nao kuvunja makundi kwani uchaguzi umemalizika ni vyema wakaenda kufanya kazi ili kuakikisha wanakitetea chama hicho kwenye Nyanja na nafasi mbali mbali.