Zinazobamba

OFISI YA WAZIRI MKUU YAIKABIDHI TASAC BOTI YA DORIA.


Na Mussa Augustine.

Ofisi ya Waziri Mkuu imekabidhi Boti ya kisasa ya  Doria ( BP SAILFISH) kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) kwa ajili ya kuimarisha doria na kukabiliana na Vitendo vya  Uharifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini.

Akizungumza leo Septemba 19,2024 Jijini Dar es salaam  katika Chuo Cha Bahari( DMI) wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya Boti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz amesema kuwa Boti hiyo  ilinunuliwa kupitia mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). 

Dkt Yonazi amesema kuwa Doria hizo ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukabialiana na vitendo vya kihalifu kama vile uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara za magendo na utoroshwaji wa nyara za Serikali. 

"Ni matumaini yangu kuwa boti hii itatimiza lengo hilo na kuimarisha juhudi za Serikali za kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika eneo letu la bahari" amesema Katibu Mkuu huyo

Nakuongeza kuwa "Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ina imani kubwa na uwezo wa TASAC katika usimamizi, uendeshaji na utunzaji wa boti hii. Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea boti hii kukabidhiwa kwa Shirika hili.

Aidha amesisitiza kuwa anaimani TASAC itaitunza vizuri boti hiyo ikiwa ni pamoja na kuifanyia matengenezo kinga kwa wakati na hivyo kuwaongezea ufanisi katika kazi zao za kila siku hususani katika ukaguzi kwa meli zinazoingia kwenye maji yetu ya ndani. 

Aidha ameiomba TASAC wakati wa Matumizi ya Boti hiyo  kuzingatia Mwongozo wa Kitaifa wa kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu wa Mwaka 2022.

"Niwaombe na kuwasihi muendelee kufanya kazi kwa karibu na Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuweza kuratibu programu za uokozi kwa majanga ya majini na usalama wa bahari kwa ujumla."amesema 
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ludovick Nduhiye amesema kuwa faida zitakazopatika kwa Wizara hiyo kupitia TASAC kukabidhiwa Boti hiyo ni pamoja na kuimarisha ulinzo katika bahari,kufanya shughuli za uchunguzi na kukusanya taarifa za kihalifu ambazo zitasaidia katika udhibiti wa shughuli haramu baharini.

Nduhiye ameongeza kuwa faida zingine ni kuimarisha utayari wa kukabiliana na shughuli haramu,kuongeza uthibiti wa ubora wa bidhaa au usafirishaji wa bidhaa hizo ,Kukabiliana na ajali za Majini ndani ya ukanda wa Tanzania,kusaidia shughuli za uokozi wa waathirika wa Majanga ya kwenye Maji kwa kuwavusha na kuwapeleka katika eneo salama pamoja na Kukabiliana na ajali za Moto kwa kuwa ina vifaa maalumu vya ajili ya kuzima moto.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini( TASAC) Mohamed Salum ameishukuru serikali kwa kuendelea kupambana na matukio haramu na yakihalifu,hivyo serikali imehakikisha Mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu unatekelezwa kikamilifu.

Aidha Salum amesema kuwa upatikanaji wa Boti hiyo umefanyika katika wakati muafaka kwani utachagiza shughuli nyingi muhimu za Utekelezaji wa vipaumbele vya Mradi wa Kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu.

"Hii Boti itasaidia Utekelezaji wa majukumu ya TASAC iliyokasimiwa kisheria,hususani jukumu la Usimamizi wa usalama ,ulinzi na utunzaji Mazingira dhidi ya Uchafuzi utokanao na shughuli za Meli ,Boti tunayokabodhiwa Leo itasaidia Utekelezaji wa jukumu hilo" amesema Mkurugenzi Mkuu wa TASA
Boti ya Dori iliyokabidhiwa kwa TASAC 

Hakuna maoni