Zinazobamba

UZINDUZI WA KITABU CHA SAMIA NA FALSAFA YA SAMIAOLOJIA UTAFANYIKA MACHI 19 MWAKA HUU


 Na Mussa Augustine 

Uzinduzi wa Kitabu cha Samia na Falsafa ya Samialojia kinatarajiwa kuzinduliwa Machi 19,2025 Jijini Dar es Salaam ambapo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anatimiza miaka minne tangu aingie madarakani.

Rais Dkt.Samia ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya uongozi wa Rais tangu Tanzania ipate Uhuru Mwaka 1961,ambapo  amekuja na Falsafa yake katika uongozi ya 4R ambayo imekuwa mkombozi kwa vyama vya siasa na watanzania kwa ujumla.

Nukuu ya"Falsafa ya 4R ambayo ni Maridhiano(Reconciliation),Ustahimilivu (Resilience),Mageuzi (Reform) na Kujenga Upya(Rebuilding)".

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Machi 2,2025 Jijini Dar es Salaam Mwandishi wa Kitabu hicho Derek K.Murusuri amesema kuwa kitabu hicho kitazinduliwa Machi 19 mwaka huu , siku ambayo aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni mwanamke wa kwanza Tanzania kushika nafasi hiyo ya Urais.
                Rais Dkt Samia Suluhu Hassan 
Mwandishi Derek.K.Murusuri amesema kwamba ameiona Falsafa hiyo ya Rais kuwa muarobaini wa utulivu zaidi Tanzania  na amani ya Afrika na Dunia .

"Katika Bara lililojaa migogoro na vita anuai,raslimali nyingi za mataifa ya Afrika zinatumika kustawisha migogoro badala ya mazao ya kiuchumi na kushindwa kuwahudumia wananchi wake ipasavyo.Mataifa mengi yanabaki katika umaskini mkubwa licha ya kuwa na raslimali asili lukuki.Falsafa ya 4R ni suluhisho", amesema Murusuri.

Aidha ,amesema uzinduzi wa kitabu hicho ni siku ambayo Rais Samia aliapishwa rasmi na katika uongozi wake ameleta mageuzi makubwa ya kisiasa ,kiuchumi na kijamii.

"Kitabu hiki ni zawadi kutoka kwa Wananchi wa kawaida walio ona,wakaguswa na utendaji wa Rais katika kuliongoza Taifa na kuwathamini watu,tukaguswa na utendaji wa Dkt.Samia Suluhu Hassan,tukaamua kuandika kitabu,si tu kwa kumpa moyo yeye bali pia kwa kuhifadhi historia ta mambi amzuri yasije yakachukuliwa na upepo",amesema

Aliendelea kwamba kitabu hiki kinafanikio mengi katika uongozi ambayo yanaweza kuigwa na mataifa mengine mbalimbali si  tu barani Afrika ,Bali pia duniani kote,

"Kitabu kinatoa mapendekezo maalum na mambo mengine muhimu yanayoweza kuwatia moyo na kuwafunda vijana wa kike na kiume,wanaotamani kuwa viongozi kupitia nyayo za Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuacha urathi katika Kila hatua ya maisha Yao",amesema

Hata hivyo amesema Kitabu hiki ni cha uongozi unaobadilisha.Uongozi wa utumishi wenye malengo yakuleta mabadiliko.Si kitabu Cha kuweka kabatini.

"Ni mwongozi wako katika utumishi wa wanadamu hapa duniani ili kuratibu uratho wako kila utakapokanyaga",amesema Murusuri.

Vilevile Murusuri ameomba niungane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Muasisi wa Taasisi ya Wanawake na Samia ambaye katika DIBAJI yake, amesema kuwa..

"Kupitia Falsafa ya 4R,Mheshimiwa Dkt
Samia Suluhu Hassan ameongeza utulivu wa nchi, maridhiano na mashirikiano kati ya Watanzania wenyewe,lakini pia kati ya Tanzania na nchi nyingine Duniani."

Alieleza kuwa kwa kuwa hii ni wiki ya wanawake,tunapoelekea kwwnye kilele chake tarehe 8 naweza kusema wanawake kuwa utendaji mashubuti wa Dkt.Samiq,kupitia falsafa hii umeiheahimisha sana nchi yetu,umewaheshimisha watanzania na hakika,umewaheshimisha wanawake,si Tanzania pekee,bali wa Afrika na Duniani kote.

Ameongeza kuwa Rais Dkt Samai  ameithibitishia Dunia kuwa uongozi hautegemei jinsia bali ni kipaji cha Mwenyezi Mungu.

Hakuna maoni