Zinazobamba

MEYA WA UKAWA UBUNGO KAMA LISSU,SOMA HAPO KUJUA

BONIPHACE   Jacob, Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaama amemtaka Rais John Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano  kuwakemea watendaji wa serikali wanaokataa kupeleka maendeleo kwenye maeneo ambayo wapinzani walishinda uchaguzi, anaandika  Irene Immanuel.
Boniphace ameyasema hayo leo huku akisema kumekuwapo na uwezeshaji hafifu wa maendeleo katika maeneo ambayo wapinzani wanayaongoza.
“Mmoja ya mtu tunaye mlalamikia sana kuwa mstari wa mbele kukwamisha miradi kwenye maeneo yanayoongozwa na  wapinzani ni aliyetajwa na Tundu Lissu, kama ndugu wa karibu wa Rais (mpwa wake),”  amesema
“Doto James akiwa Naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango ndiye alikwamisha mradi wa kujengewa kiwanda cha mbolea, kule Mabwepande.” amesema
Amesema wakati akiwa Meya wa Kinondoni, alifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo, lakini James alisababisha kunyimwa ufadhili wa kiwanda chenye thamani ya Sh. bilioni 3.2 kutoka kwa serikali ya Ujerumani.
Alimtaja  James kuwa ndiye anayelalamikiwa na Bella Bird, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa kuchelewesha kwa makusudi mradi wa uboreshaji wa jiji la Dar es salaam kwa halmashauri zote za wapinzani.
Amesisitiza umuhimu wa Rais John Magufuli, kujitokeza hadharani  kuwakana au aseme kawatuma wote wanaokwamisha miradi kwenye halmashauri za wapinzani huku akiwataka wananchi kutokubali ubaguzi huo.