Zinazobamba

KASI YA DC HAPI NI KIBOKO,ATOA ONYO KALI KWA WANASIASA,SOMA HAPO KUJUA

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amesema mwanasiasa atakayeingilia  mgogoro wa ardhi Katika Mtaa wa Nakasangwe, Kata ya Wazo atakwenda na maji kwani serikali ipo kwa ajili ya kulishughulikia.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akizungumza leo na wakazi wa Mtaa wa Nasarangwe, Kata ya Wazo jijini Dar es Salaam. 

Kauli hiyo meitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wa mtaa huo kuwaeleza walipofikia katika kutatua mgogoro huo uliodumu kwa miaka 13 ukihusisha wamiliki wamashamba na wakazi hao.

“Hakuna mtu yeyote atakaye tatua mgogoro huu isipokuwa serikali, hivyo wanasiasa wanatakiwa kufanya kazi zao na wasiingilie hili kwani hawana ubavu,” alisema Hapi.

Akizungumzia kuhusu mgogoro huo amesema kuwa baada ya majadiliano baina ya pende hizo mbili zilizokuwa na mgogoro (wamiliki wa mashamba na wakazi) walifikia mwafaka wa kwamba eneo hilo halitakuwa na mashamba na badala yake ardhi hiyo itapimwa na kugawanywa kwa viwanja na kila mwananchi kupatia na hati ya umiliki.

Aidha ameeleza kwamba katika utekelezaji wa upimaji na ugawaji wa viwanja kampuni ya Afro Map imepewa kazi hiyo na kuagizwa kukamilisha ndani ya miezi mitatu badala ya miezi nne iliyokuwa ikifahamika hapo awali.

Mkuu huyo wa Wilaya pia amewaonya watumishi wa Halmashauri hiyo kutojaribu kuingiza majina mapya kiujanja katika ugawaji wa viwanja hivyo na kusisitiza kwamba watakao husika ni wakazi tu waliokuwepo katika uhakiki.

Ametoa rai pia kwa watu ambao wana maeneo yasiyo na mgogoro nao watoe ushirikiano katika zoezi hilo kwani baada ya upimaji utasaidia kupata maeneo ambayo yatasaidia kutolea huduma nyingine kama za shule, afya na kadhalika.

Ameongeza kuwa kwa watu wenye mashamba wakate viwanja na kuwauzia wengine au kama wana watoto wawagawie ili wayaendeleze kutokana na kwamba Wilaya hiyo haitaka kwa hivi sasa kuwa na mashamba katika eneo hilo isipokuwa makazi tu.

Hapi ameonya watakao pewa viwanja na kushindwa kuvindeleza wstspokonywa. Na aliagiza kusitisha shughuli zote za kuuza au kuendeleza ardhi hiyo hadi shughuli ya upimaji na ugawaji wa viwanja ukamilike.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Wazo Joel Mwakalebela amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuchangia gharama ugawaji wa viwanja ili zoezi hilo lisikwame.

Ametoa rai kwa watu wasio husika katika mgogoro huo wapimiwe maeneo yao pia kwani itasaidia kupata ardhi kwa ajili  huduma nyingine kama ya elimu na afya.









Ab