Zinazobamba

DEMOKRASIA INAZIDI KUPOROMOKA--PROF LIPUMBA.

Na Mussa Augustine.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi(CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba amesema kwamba Demokrasia imeporomoka Duniani kote.

Prof.Lipumba ametoa matamshi hayo leo Januari 8,2025 Jijini Dar es salaam wakati akifungua Kikao Cha baraza kuu la Chama hicho,nakubainisha kuwa jukumu la kulinda Demokrasia hapa nchini niya Watanzania wote.

Aidha amesema kwamba kwa upande wa Tanzania kuporomoka kwa Demokrasia imejidhihirisha katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliyofanyika Mwaka 2024 hivyo amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anajukumu la kuhakikisha dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa 2024 na 2020 hazijitokezi tena katika uchaguzi mkuu unaofanyika Mwaka huu Nchini humo.
" Hali ya Demokrasia Duniani ilikua ikiporomoka ,wataalamu wa mambo ya Demokrasia wanaonesha katika tafiti tangu Mwaka 2006 ,Demokrasia imekua ikiporomoka Duniani" amesema  Prof.Lipumba

Nakuongeza kuwa ,hata Marekani ambapo pamoja na mapungufu mengi ndiko utaratibu wa Demokrasia ulipoanza kwa kuweza kuchagua viongozi wa kuwawakilisha wananchi nako Demokrasia imekua ikiporomoka."
Aidha ameongeza kuwa hata uchaguzi uliopita wa Marekani wa kumchagua Rais Donald Trump ambaye Mwaka 2020 aliyakataa matokeo ya uchaguzi inaonesha namna Demokrasia ilivyoporomoka Nchini humo.

Ameongeza kuwa jukumu la ujenzi wa Demokrasia hapa nchini nila Watanzania wote,nakusisitiza kuwa Demokrasia imekua ikiporomoka.

Profesa Lipumba amedai kwamba kutokakana na kuonekana  kuporomoka Demokrasia nchini,amemsihi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kusimamia ipasavyo falsafa yake ya 4R ili kuendelea kuimarisha Demokrasia nchini.




Hakuna maoni