Huyu ndie Mkurugenzi mpya wa FBI
Christopher Wray
Washington.Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kumthibitisha Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI.
Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipoondolewa kwenye wadhifa huo na na Rais Donald Trump Mei.
Aliondolewa baada ya uchunguzi aliokuwa akiufanya kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi Trump.
Christopher Wray ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa mahakama ya nchi hiyo ambaye amefanya kazi chini ya Rais George Bush.
Huyu ndie Mkurugenzi mpya wa FBI
Reviewed by Unknown
on
18:08:00
Rating: 5