WAZIRI MWAKYEMBE ASEMA HAYA BAADA YA KIFO CHA MKEWE,SOMA HAPO KUJUA
Leo Jumatano ya July 26 ikiwa ni siku 11 zimepita toka utokee msimba wa mke wa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe, leo ameongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam.
Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan.
Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
==>Ulizisoma hizi??
1.Serikali yatangaza nafasi 150 za kazi za Udereva wizara mbalimbali.
2.Nafai 48 za Kazi Toka Tanzania Public Service College (TPSC)
==>Ulizisoma hizi??
1.Serikali yatangaza nafasi 150 za kazi za Udereva wizara mbalimbali.
2.Nafai 48 za Kazi Toka Tanzania Public Service College (TPSC)
Mbali na hao, Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela Mkoani Mbeya, amewashukuru viongozi wote wa dini akiwamo Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zuberi na maaskofu.
"Wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mwisho kabisa Wanakyela kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kigumu," amesema Dk Mwakyembe.