Mwanamke Mmoja Auawa Kibaha....Polisi Watangaza Vita
Baada ya mkazi wa Mharani kwa Matiasi wilayani Kibaha kukutwa amefariki dunia kwa kuuawa na watu wasiojulikana jana majira ya saa moja usiku, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana ametangaza mapambano makali ya kuwatia nguvuni wahalifu.
Kamanda Shana amesema kuwa mwili wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Omari (31) ulikutwa nje ya nyumba anayoishi mbele kidogo umbali wa mita 40 akiwa anavuja damu nyingi sehemu za usoni na jereha kichwani upande wa kushoto huku muuaji akiwa bado hajafahamika.
"Kufuatia tukio hili jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaweza kuwabaini waliojihusisha na tukio hilo, Pia wananchi wanatakiwa watoe ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na hayo Kamanda Shana amewatahadharisha watu wote wanaojishughulisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani jeshi limejipanga kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria