Zinazobamba

Anudha Limited: Wasambazaji wa vifaa vya Hospitali wanaotimiza kauli ya "Hapa kazi tu" kwa vitendo...yajivunia miaka 81 ya utoaji huduma kwa watanzania

Baadhi ya vifaa vya Afya vilivyopo katika banda la anudha limited, vikiwa katika maonesho. Vifaa hivyo vilionyeshwa katika mkutano wa wadau wa Afya uliofanyika jijini Daresalaam.
Vifaa mbali mbali vya Afya vikionekana katika banda la anudha limited.
"Linapokuja suala la usambazaji wa vifaa vya Hospitali iwe ya Serikali au  binafsi, mashirika ya umma na hata watu binafsi siku zote kumbuka anudha limited, sisi ni watu mahususi ambao tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa watanzania kuanzia uuzaji na utoaji elimu na ufundi wa vifaa vyetu tunavyouza"
Tupo katika soko toka mwaka 1936... lakini tumekuja kufahamika zaidi mwaka 1996 ambapo tulianza kutanua mbawa zetu na kufanya biashara ya kuuza vifaa aina zote za Hospitali...kwa kweli tunaweza kusema huduma zetu zimekuwa zikipendwa na wateja wetu...ukihudumiwa na sisi hutajuta.

Ni maneno kutoka kwa mtaalamu wa vifaa vya theatre wa Kampuni ya Anudha Limited, Bw.Soko Protas wakati akifanya mazungumzo na Mwandishi mwandamizi wa Mtandao huu.

Aidha akielezea sababu za wao kuhudhulia katika mkutano huo, Protas amesema wao kama kampuni wanapaswa kutoka hadharani na kuzungumza ni kwa jinsi gani wanafanya kazi zao...pia kuonyesha mitambo mipya ambayo wanayo itakayoweza kukidhi haja ya Hospitali zetu.
"sisi tunafanya kazi na makampuni makubwa duniani...wanatengeneza sisi tunasambaza hivyo ni busara watu wakafahamu kuhusu huduma bora inayopatikana kwetu".

Anudha Limiteda ni miongoni mwa makampuni yanayosambaza vifaa vya Afya hapa nchini, ambayo hufanya kazi na Hospitali za Serikalia pamoja na binafsi, pamoja na mashirika ya dini.
  Bw. Soko Protas, alisema kuwa vifaa wanavyosambaza katika hospitali wanaagiza kutoka mataifa mbali mbali mkubwa.