Zinazobamba

MTOTO WA KARUME AMCHANA JPM,SOMA HAPO KUJUA

FATUMA Karume, wakili wa Tundu Lissu, Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kila mtu ana haki ya kumkosoa Rais, anaandika Hellen Sisya.
Wakili huyo ameyasema hayo nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ambapo Lissu amefikishwa siku ya  jana akishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi ambayo imeleta chuki katika jamii.
“Kinyago ulichokichonga mwenyewe kweli kikutishe? Maana tukumbuke mwaka 2015, Rais John Pombe Magufuli kaja kutuomba sisi kura.
Kwa hivyo sisi tuna haki leo ya kumkosoa, na hiyo haki tutaipigania.” amesema wakili huyo.
Aidha, wakili huyo alisisitiza kuwa lengo lao lilikuwa ni mteja wao kufikishwa mahakamani, na hilo limetimia.
Hivyo kuwataka wananchi kusubiri hiyo tarehe 27 ambapo uamuzi kuhusu dhamana ya mteja wake utatolewa.
Katika kesi hiyo Mawakili wa upande wa jamhuri walitoa hoja za kupinga dhamana ya Lissu, ambapo mahakama imesema kuwa itatoa uamuzi kuhusiana na dhamana hiyo kesho kutwa hivyo kusababisha Lissu kurejeshwa rumande.