RAIS MAFUFULI AWAANGUKIA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
RAIS John Magufuli, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Watanzania kuwa na mioyo ya kuvumiliana, anaandika Hellen Sisya.
Rais Magufuli ameyasema hayo mapema leo hii akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida na kusisitiza kuwa kila mmoja anatakiwa kuilinda amani.
“Niwaombe Watanzania, tuwe na mioyo ya kuvumiliana, tuitunze amani yetu.” alisema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa suala la kulinda amani ni kila mmoja wetu na kuwataka watanzania kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.
Kauli ya Rais Magufuli imekuja wakati ambao viongozi wa kisiasa wa kambi ya upinzani wakikamatwa mara kwa mara kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi, hatua inayoonyesha kuwa bado hakuna uvumilivu wa kisiasa hapa nchini.
Rais Magufuli amekuwa katika ziara ya kikazi kwa siku kadhaa sasa akitembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Kigoma, Tabora na leo ndiyo alikuwa anahitimisha ziara hizo mkoani Singida