Zinazobamba

CHADEMA WAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA

MAWAKILI wanaowatetea wanachama 54 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), wameshinda pingamizi la Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Geita, Mponjoli Mwabulambo, katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kufanya mkutano wa ndani kinyume cha Sheria, anaandika Irene David.
Wiki mbili zilizopita wanachama hao walikamatwa na kupelekwa polisi na hatimaye kufikishwa mahakamani ambapo OCD aliwakatalia dhamana dhidi yao na hivyo kubaki gereza la Biharamulo kwa wiki mbili.
Hii leo mawakili hao wameshinda pingamizi hilo na hivyo wanachama hao wataachiliwa kwa dhamana iliyo wazi na taratibu za kuwadhamini zinaendelea.