MBUNGE KUBENEA ALIAMSHA 'DUDE' MAHAKAMANI DODOMA,SOMA HAPO KUJUA
MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imepiga kalenda kesi ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea hadi Agosti 23 Mwaka huu kutokana na uchunguzi wa kesi hiyo kutokamilika, anaandika Dany Tibason.
Mbunge huyo anashitakiwa kwa kosa la jinai ambalo anadaiwa kumshambulia Mbunge wa viti maalum (CCM), Juliana Shonza.
Akisoma kesi hiyo leo mbele ya Mahakama hiyo,wakili wa serikali Foibe Magili amesema kuwa uchuguzi wa kesi hiyo haujakamilika na hivyo kumuomba Hakimu James Karayemaha aisogeze mbele.
Kwa upande wake Hakimu James Karayemaha aliridhia ombi la wakili wa serikali na hivyo kuiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 23 Mwaka huu.
Hata hivyo Mshitakiwa Saed Kubenea amesema kuwa utaratibu wa kisheria bado siyo mzuri ni vyema kesi hiyo ingebaki polisi hadi hapo upepelezi utakapokamilika na kwamba ni matumizi mabaya ya rasilmali za serikali.
Aidha, ameiomba serikali iangalie mambo hayo kwa kina na haina haja ya kukamata watu pale inapoona haina upelelezi wa kustosha.
Naye wakili anayemtetea mshitakiwa Kubenea, Isaac Mwaipopo amesema kuwa wao bado wanasubiria upelelezi ukamilike kwani wana imani na Mahakama.
Mheshimiwa Kubenea anakabiliwa na kesi ya shambulio kinyume cha Sheria kifungu namba 240 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Juali 3 mwaka huu katika eneo la Bunge Mjini Dodoma.