Zinazobamba

Siku Hizi Wazee Wako Shapu Kuliko Vijana: Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi, na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi, na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30.

Rais John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani hao ndiyo viongozi wa kesho.

Rais amezungumza hayo jana  wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini Tabora, ambapo aliweka wazi kwamba wanaowapa mimba watoto wa shule siyo  vijana pekee bali wapo wazee nao wameingia kwenye mkumbo huo hali ambayo inawafanya mabinti washindwe klumaliza elimu ya sekondari.

“Wazee siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao.

".....Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.

Pamoja na hayo Mhe. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa kitanzania elimu.

"Tumeamua kutoa elimu ndiyo maana tumetenga bilioni 18.777 tunataka watoto wasome na wasipate mimba, naomba wajiepushe na mimba mpaka watakapotimiza malengo yao," aliongeza.