KAFULILA ASEMA HAYA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMSIFIA,SOMA HAPO KUJUA
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kumpongeza David Kafulila kwa kuibua sakata la la IPTL lililowahusisha vigogo kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo wanasiasa na viongozi kutoka Serikalini.
Kafulila ambaye alitangaza kukihama chama chake cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maenfdeleo (CHADEMA), amesema kuwa amefurahishwa na kauli ya Rais Dkt. Magufuli kuhusu hatua alizochukua kuibua kashfa ya Escrow.
“Nimefurahishwa kuona mkuu wa nchi ameguswa na kutambua mchango wangu katika vita hii hatari ya ufisadi wa IPTL/Escrow kwakuwa imekuwa ikilitafuna taifa kwa muda mrefu sasa,”amesema Kafulila.
Aidha, amesema kuwa vita hiyo siyo ya kichama hivyo kila Mtanzania anatakiwa kuunga mkono ili kuweza kutokomeza na kuwakamata wale wote waliohusika na ufisadi huo ambao umeiliingizia taifa hasara kubwa.
Hata hivyo, ameongeza kuwa anatamani kuona hakuna jiwe lianalobaki katika ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ikwemo waliobeba mabilioni katika Lumbesa kutoka katika Benki ya Stanbic ambao hawajawahi kutajwa hadharani.
Akijibu swali kama sakata la Escrow ndilo lililosababisha yeye kushindwa kutetea jimbo lake, Kafulila amesema vita hiyo imemgharimu mambo mengi huku jimbo hilo likiwa ni sehemu moja,
“Jimbo hilo sikushindwa bali nilinyang’anywa baada ya kuibiwa sana ikashindikana. Nilinyang’anywa na rekodi zipo na ninaweza kuzionyesha na ushahidi wa nguvu zilizotumika kuninyang’anya jimbo hazikuwa nguvu za kawaida,” amefunguka Kafulila.
Akizungumza jana na wakazi wa Kata ya Nguruka, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, Rais Magufuli alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki itakayompeleka motoni.
Alisema anatambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli, hivyo anampongeza sana na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyoni.
Aliongeza kuwa wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa mno na Kafulila alisimama kutetea Umma wa Watanzania.
“Wakamtisha wengine hadi kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili sasa, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu kuwatumikia Watanzania,” alisema Rais Magufuli.