LHRC YAKUMBUSHIA TEGETA ESCROW-; LUGUMI, RICHMOND NA UNUNUZI WA RADA...WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUCHUKUA HATUA DHIDI YA KASHFA HIZO
KITUO
CHA SHERIA na haki za binadamu (LHRC) kimeikumbusha serikali kuhusu kuchukua hatua dhidi ya kashfa ambazo
zimesababisha Serikali hasara ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, kashfa
inayohusishwa na Kampuni ya Lugumi, kashfa ya Richmond, kashfa ya uwepo wa
harufu ya rushwa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi
ya jamii …mathalani mradi wa NSSF kigamboni pamoja na suala la Vitalu vya
uwindaji na umiliki wake.