Zinazobamba

KAMPUNI YA SIMU YA ITEL YATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA,SOMA HAPO KUJUA

Pichani kushoto ni Balozi wa Kampuni ya simu Itel ambaye pia ni staa wa Bongo Muvi,Iren Uwoga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kampuni hiyo kutoa msaada wa kwenye kituo cha Watoto Yatima kilichopo Sinza Jijini Hapa
Katika kuelekea mwisho wa mwezi mtukufu wa ramadhani  kwa mwaka 2017,kampuni ya simu ya  ITEL kwa Kushirikiana na Balozi  wa kampunio hiyo IRENE UWOYA imetoa msaada wa chakula  kwa  watoto hasa wenye mahitaji maalum katika kituo cha kulelea watoto yatima kinachofahamika kwa jina la KUHAMA kilichopo Jijini Dar es salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dasr es salaam uwoya amesema lengo la kutoa msaada huo kwa watoto hao ni kuonesha upendo, furaha na ushirikiano katika kipindi hiki cha  maandalizi ya sikukuu ya Eid l fitri.
Aidha balozi huyo ameziunga mkono jitihada zinazofanywa na kiutuo hicho cha kulelea watoto yatima pamoja na vituo vingine katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakuwa na furaha na kupata mahitaji yote wanayostahili.
Sehemu ya Misaada iliyotolewa na Kampuni hiyo bomba ya simu 


Kwa upande wake Katibu mtendaji wa kituo hicho cha kulelea watoto yatima HASSAN HAMISI  ameeleza baadhi ya changamoto  zinazowakabili katika kituo hicho ni pamoja na ,malezi ya watoto hao,upungufu wa vifaa vya shule,kutokuwa