WATENDAJI WA MAGUFULI WAANZA KUTOFAUTIANA,NI KUHUSU SAKATA LA MAKONDA NA WASANII WATUMIAJI UNGA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii
wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda
Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati
akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku
nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo
wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa
mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID,
Tunda, Babuu wa Kitaa n.k
Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu
suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na
ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo
msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo
hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu
wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike
kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na
kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya
kuwasaidia.
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la
jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga
maadili ya watoto.