PROFESA LIPUMBA AWEWESEKA,AIBUKA NA KUKANUSHA KUWA YEYE SIO SHUSHU WA SERIKALI,SMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa
Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma za kuwa na ukaribu unaotia shaka kati yake na
serikali na kutolea ufafanuzi ishu mbalimbali zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo
ya kuchepusha ruzuku ya chama.
Mwenyekiti huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama
vya Siasa amesema kinachodaiwa kuwa ni ukaribu wake na serikali, siyo sahihi
kwa kuwa yeye huwa anaalikwa tu kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo
hawezi kukataa mwaliko.
"Kwa mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya
serikai, labda Rais anazindua kitu, au sherehe za kitaifa na Rais yupo
utakataaje" Amesema Lipumba.
RUZUKU
Suala la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni
jambo linalodaiwa kuwa ushahdi wa Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali,
ambapo amesema ilikuwa ni lazima iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama
Mwenyekiti wa chama wa kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye
aliyekuwa mtia sahihi katika masuala ya fedha.
Pia sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku
amesema ni mahitaji ya chama kwa kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo
kilihitaji fedha kwa ajili ya shighuli mbalimbali.
" Kuhusu ruzuku, nilikuwa
nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana Bashange, kwahiyo hakuwa tena
signatory wetu, kwa nafasi yangu kama mwenyekiti niliona hafai, tukajitahidi
kufungua akaunti nyingine lakini haikuwezekana. Ikabidi Naibu Katibu Mkuu
ambaye ndiye anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo ofisini, aandike
barua ya kuomba ruzuku kwa ajili ya mahitaji tuliyokuwa nayo"
Ameeleza Lipumba
Lipumba ameendelea kusema "Tukapeleka
taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu Katibu Mkuu akaandika barua kwenda kwa
Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie kwenye akaunti nyingine, na hilo
likafanyika"
MIKUTANO
Kuhusu yeye kuruhusiwa kufanya M ikutano, huku
Katibu Mkuu wake akizuiliwa, hususani tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba
amesema hata yeye alipokwenda Mtwara hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa
kimempeleka, na badala yake aliishia kufanya mikutano ya ndani, huku
akibainisha kuwa kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda bila kutoa taarifa kwa
kiongozi wa wilaya.
"Nimekwenda Mtwara, nilikaribishwa
na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni kufungua matawi, lakini polisi
wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano ya nje, nikafanya mikutano ya
ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila kumtaarifu kiongozi wa wilaya". Amesema
ULINZI
Lipumba aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja
cha TV, amekanusha taarifa za kupewa ulinzi na serikali na kufafanua tukio la
kupigiwa saluti na askari, akisema kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali
diwani wa eneo ambalo yeye alishiriki kufanya usafi.
"Pale Buguruni, tulikuwa katika
usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile, askari walikuwa wakiangalia usalama,
na alipotokea diwani wa eneo lile, askari walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu
wa eneo lile, siyo mimi"
Kitendo kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti
Prof Lipumba
Katika hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua
Maalim Seif kama Katibu Mkuu halali wa CUF, huku akimtaka amfuate ili
wamalize tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.