MFANYABIASHARA MO DEWJI.MATATANI KWA KUKWEPA KODI,SOMA HAPO KUJUA
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya
kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni,
mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.
Katika
hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za mkoa wa Dar es
salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo
Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada Hotel
anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji
kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika
Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.
Makampuni
hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na
endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili
kufidia gharama wanazo daiwa.
Serikali
kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha
oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na
mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akiongea
kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17
Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango
la Ardhi.
Wizara
haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa
sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi
ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa
sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.
Baadhi
ya watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment na baadhi ya Waandishi wa
Habari wakiwa nje ya Ofisi ya Mohammed Enterprises iliyopo jingo la
Golden Jubilee mara baada ya wafanyakazi wa Mohammed Enterprises
kukimbia.
Wafanyakazi
wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya
kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya
Msolopa Investment.
Watumishi
kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana
na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka
ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha
notisi ya madai ya kodi ya ardhi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia
Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi
hata kama ni Taasisi ya serikali.
Hassan I. Mabuye
Information Officer
The Ministry of Lands, Housing
and Human Settlements Development
Dar es salaam, Tanzania