RAIS MAGUFULI AJITOSA VITA YA MADAWA YA KULEVYA,APIGILIA MSUMARI ,SOMA HAPO KUJUA
]
Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na
usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya bila kuangalia umaarufu au
cheo cha mtu.
Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa
akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Vanance Mabeyo pamoja na viongozi wengine
wa majeshi, na mabalozi.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kwa hatua nzuri aliyoichukuwa ya kuwasimamisha kazi Askari Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa
mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina
yao.
"Najua IGP Mangu watu walikupigia
simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa
IGP.
"Vita ya dawa za kulevya haina cha
umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu
mkamateni.
"IGP nakuagiza kamata watuamiaji
wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama
njugu."Amesema Rais Magufuli
Akizungumzia suala la uendeshaji wa kesi za dawa
kulevya, Rais Dkt Magufuli amemwambia Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji
Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa kesi hizo zinaendehswa taratibu sana huku
akitolea mfano wa mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya aliyekamatwa
mkoani Lindi lakini hakuwahi kufikishwa mahakamani.
"Kuna mfanyabiashara maarufu wa
dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa
mahakamani" Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema kuwa vita ya dawa za
kulevya si ya Paul Makonda peke yake bali ni ya Watanzania wote huku akivitaka
vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kushirikiana kutokomeza tatizo hili
linalopelekea kupoteza nguvu kubwa ya taifa.
Kauli hii ya Rais Magufuli inakuja ikiwa ni siku chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atangaze vita dhidi ya watu wanaohusika na dawa za kulevya akianza kwa kutaja majina yakiwemo ya askari na ya wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde n.k.
Siku tatu baada ya Makonda kuwataja watuhumiwa hao, IGP Ernest Mangu alichukua hatua ya kuwasimamisha askari 12 waliotajwa na kuahidi kuchukua hatua zaidi, jambo ambalo limepongezwa na Rais Magufuli na kumueleza kuwa endapo asingechukua hatua hiyo, angejua kuwa na yeye anahusika.