RC MAKONDA AIBUKA TENA NA HILI,SASA ATANGAZA KIAMA ,SOMA HAPO KUJUA
Leo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
amezungumza akiwa kituo cha kati cha Polisi Dar es salaam pembeni ya Kamishna
Simon Sirro kuhusu ishu ya dawa za kulevya inayoendelea kwenye headlines.
Mambo aliyoyasema mkuu wa mkoa Paul Makonda
leo ni kutoa siku kumi kuanzia kesho February 7 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa,
Wazazi na Watumiaji na Wafanyabiashara.
==>Natoa siku 10
kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es salaam kutoa taarifa za
mtaa wake juu ya dawa za kulevya.
==>Natoa siku 10
kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za
kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa….. tukikukamata baada ya siku kumi na
mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie
dawa za kulevya.
==>Natoa siku 10 kwa
Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa
kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo
Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi
kelele nyingine zinatupa hamasa