Zinazobamba

PROFESA LIPUMBA AWASHUKIA WANAOUBEZA MUUNGANO,PIA AMSIHI MAALIM SEIF KUREJEA OFISINI SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WANACHAMA cha wananchi (CUF) wametakiwa kutoutumia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho ili kuvunja muungano  uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa  chama hicho ambaye anatambulika na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini,Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Ambapo Profesa Lipumba amesema inasikitisha kuona wako baadhi ya viongozi wa chama hicho wanautumia mgogoro wa kikatiba unaendelea ndani ya chama hicho ili kuharibu muungano uliopo jambo analodai halifai kufanywa na viongozi wa chama hicho kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar.
“Kukweli ukitoa Chama cha Mapinduzi (CCM) chama kingine ambacho kinauenzi muungano ni Chama cha CUF,hivyo nashangaa wapo viongozi wanaobeza muungano huu,hivyo lazima tuwapinge watu hawa’amesema Profesa Lipumba.
Hata Hivyo,Lipumba ameendelea kumsihi katibu mkuu wa Chama hicho,Maalim Seif kurejea ofisini ili waweze kukijenga chama hicho.
Amesema kitendo cha Katibu mkuu huyo kutokuja ofisini kunazidi kiweka vibaya chama hicho na kushindwa kueleweka kwa jamii jambo analomsihi katibu mkuu huyo kutafakari uamuzi wake wakutokuja ofisini