MAHAKAMA YAAMUA HAYA KWA WASANII WAPWIA MADAWA YA KULEVYA,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
leo imetoa maamuzi kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu
tuhuma zinazomkabili Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana
ya shilingi milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa
mwezi kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja
mwaminifu.
Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani
Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani