NAIBU SPIKA ALIANZISHA TENA,WABUNGE WA UKAWA WAMSUSIA BUNGE LAKE,SOMA HAPO KUJUA
Wabunge wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni
katika kikao kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao
kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.
Wabunge waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi
wa Bunge na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima
Mdee, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.
Wabunge hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu
Spika kuhusu muongozo ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu
utaratibu uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mara baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa
wabunge hao watatu bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua
kutoka kama ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga
utaratibu wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.
Nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto
Kabwe , amesema wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa
kukamata wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na
vikao vya bunge lakini mapambano yataendelea.
"Kesho tunarudi bungeni, lakini
mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa utaratibu huu wa kuvizia wabunge
kwenye milango ya bunge bila taarifa rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge
sababu za kukamatwa kwao siyo sawa. Tukilifumbia macho litakuja kumtokea mbunge
yoyote hata wa CCM" Amesema Zitto