WAZIRI NCHEMBA AGUSWA NA HALI MBAYA YA MSANII CHID BENZI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
ameguswa na hali ya uathirika wa matumizi ya dawa za kulevya inayomtesa rapa
Chid Benz na kulazimika kufika nyumbani kwao kuzungumza na mama yake mzazi.
Chidi Benz anayemiliki tuzo kadhaa za muziki
alijikuta amenasa kwenye mtego wa matumizi ya dawa za kulevya ambao sio tu
ulimuondoa kwenye maisha ya muziki bali pia uliidhoofisha afya yake na kuuondoa
kabisa mwili wake wa ‘chuma’.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Waziri Nchemba
ameeleza kusikitishwa na hali ya Chidi Benz na kutumia nafasi hiyo kuwataka
wale wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuacha mara moja
kwani Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kupambana nao.
Hivi ndivyo alivyoandika:
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii
Rashid Makwilo “Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za
kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku
wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya
magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika
awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna
yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu
wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara
haramu ya madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada
wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua
matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.