WAZIRI MKUU AWAMALIZA RASMI WALIMU WA SANAA WANAOSUBILIA AJIRA SERIKALINI,,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali
haitoajiri walimu wa sanaa kwa madai wametosha,huku akisema serikali ipo katika
hatua za mwisho wa kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati elfu nne tu,
Waziri mkuu ametoa msimamo huo wa serikali leo
jijini Dar es salaam wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya
mpya ya kigamboni yenye lengo la kukagua shughuli mbali mbali za
maendeleo,,Waziri mkuu amesema kwa sasa serikali imebaini kunauhaba wa walimu
wa sayansi na hisabati hivyo serikali itaajiri walimu hao tu,
“Nataka niwambie kwa sasa serikali itaajiri walimu wa sayansi tu.kwani walimu wa sanaa wametosha nchini hatutaajiri kwa sasa'”amesema Majaliwa,
,Hata hvyo Majaliwa amesema kwa sasa serikali imeanza kutoa kibali cha kuajiri watumishi kwenye idara zote za serika ili kujaza nafasi za watumishi hewa waliondolewa,
Kauli ya waziri mkuu ni kama inaibua mjadala
mpya,baada ya bajeti ya serikali 2016-2017 kusema serikali itaajiri walimu 35000,lakini
kwa sasa serikali imesema itaajiri walimu elfu4000 tu,huku ikibaki miezi mitatu
ifikie ukomo