SERIKALI YAPELEKA KILIO KWA WATUMISHI WA UMMA,YAFUTA POSHO RASMI,SOMA HAPO KUJUA
Serikali ya awamu ya tano imeendeleza desturi yake
ya kubana matumizi, ambapo leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefuta rasmi posho
zote za watumishi wa Umma na kuelekeza posho hizo kufanyiwa miradi mbalimbali
ya Maendeleo katika Halmashauri husika nchini.
Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo 3 Januari
2017, katika ziara yake iliyofanyika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akieleza jambo hilo amebainisha: “Kuanzia Januari
hii mtu asipewe posho ya aina yoyote ile, nafuta posho zote ziende katika
miradi ya maendeleo,” amesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Majaliwa ameagiza Halmashauri zote
nchini kusimamia fedha za miradi ya maendeleo za madiwani.
“Sasa hivi madiwani hakuna kupewa fedha za miradi ya
maendeleo mkononi, bali wawasilishe vipaumbele vya miradi yao ili halmashauri
husika isimamie malipo yake kwa ajili ya kuepuka migogoro,” amesema.
Pia, Majaliwa amezipiga marufuku kampuni za
watumishi wa umma kufanya kazi katika halmashauri wanazofanyia kazi.
“Madiwani kama mna kampuni haziruhusiwi kufanya kazi
katika halmashauri walizopo ili kuondoa upatikanaji wa dhabuni za upendeleo
kitendo kinachoshusha ufanisi wa kazi,” amesema.
Amezitaka halmashauri zote nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji
mapato ya kodi na yasiyo ya kodi.
” Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku
kwa halmashauri zote nchini kulingana na bajeti itakavyo ruhusu, tunataka
halmashauri zitekeleze miradi yake ipasavyo,” amesema.
Amesema kwa sasa Halmashauri za Jiji la Dar es
Salaam zinateketeza fedha nyingi kwa ajili ya posho badala ya kutekeleza miradi
ya maendeleo ambapo Halmashauri za wilaya ya Temeke na Kigamboni zinatumia laki
5 kila mwezi kwa ajili ya posho za kuchochea maendeleo ya madiwani
wakati Ubungo ikitumia milioni 55 ambayo ni sawa na
zaidi ya milioni 600 pamoja na posho za vitafunwa milioni 300 kwa mwaka huku
kinondoni ikitumia milioni 780 kwa ajili ya posho ya maendeleo na milioni
390 kwa ajili ya posho ya bites kila mwaka.