MBUNGE LEMA NIFUNGU LA KUKOSA MAHAKAMANI,AKWAMA TENA,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa
kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya
kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma
Maghimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri
iliyopinga Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama
ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa
lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri
iliwasilisha notisi ya mdomo.
Baada ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi
akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya
Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada
ya mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya
Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria
kutoa uamuzi wa rufani hiyo.