IGP MANGU AVUNJA UKIMYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA ZANZIBAR,ATUMA MAOFISA WA POLISI,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu
ametuma timu ya Maofisa wa Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii
Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi
juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo
vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Timu hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo
vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia
vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani.
IGP Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za
kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu
hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.