WANAHARAKATI WAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI KWENYE KESI YA SHERIA YA MAKASA YA MTANDAO,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya
kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali
miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao
kilichobatilishwa.
Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu
vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa
matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.
Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba,
iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha
Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.
Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John
Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu
cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.