RAIS MAGUFULI AWATOLEA "NJE" WANAKOSA CHAKULA,ASISITZA SERIKALI YAKE HAITA MSAIDIA MTU MWENYE NJAA,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amezuia serikali
kupeleka chakula cha msaada wilayani Misenyi mkoani Kagera kwa madai kuwa
wilaya hiyo haina sababu ya kukumbwa na tatizo la njaa.
Rais Magufuli amekataa serikali kupeleka chakula cha msaada katika wilaya hiyo na kusema haikubaliki kwa eneo hilo lenye mvua za kutosha na hali nzuri ya kilimo na kwamba haiwezekani kulia njaa wakati kuna uwezekano wa kuzalisha kwa ajili ya chakula.
Amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika
kituo cha afya cha kata ya Ishozi Wilayani Misenyi Mkoani Kagera ambapo yupo
kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua maendeleo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli, amesema kuwa
serikali haitaweza kujenga makazi ya kila mwathirika wa tetemeko mkoani Kagera
kwa kuwa ina jukumu la kujenga miundombinu itakayokuwa na manufaa kwa jamii
nzima kama Zahanati, Shule na barabara.
Amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao nyumba zao
hazikuharibika kiasi kikubwa lakini wakadanganywa na baadhi ya watu kuwa
watajengewa hivyo wakazibomoa kwa kutaka kujengewa nyumba mpya.a.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga
makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha
Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi
mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha
Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.