WALIMU WAMPA MASHARTI MAGUMU JPM NA SERIKALI YAKE,WASEMA WASIPO LIPWA MADENI YAO WATAFANYA MAAMUZI MAGUMU,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
Chama cha walimu nchini (CWT) kimeitaka serikali
kuwalipa madai yote ya Walimu yanayofikia trion 1.06 kabla ya mwisho wa mwezi
huu ambapo baraza la uongozi la CWT halijakutana ili waweze kujadili na
kutoa maamuzi magumu endapo deni hilo lisipolipwa.
Hata hivyo chama hicho pia kimeitaka serikali kuacha
kuwahadaa watanzania kwa kusema walimu wa sanaa wapo wa kutosha ,huku wakiitaka
serikali iseme ukweli kwani bado kwenye shule hapa nchini kuna uhaba mkubwa wa walimu wa
sanaa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu
Katibu Mkuu wa (CWT) Ezekiah Oluoch wakati wa mkutano na waandish wa
Habari ambapo amesema chama hicho kimefanya Mazungumzo na ofisi ya waziri
mkuu,naibu waziri wa elimu Mhandisi Stella Manyanya pamoja na kukutana na
makatibu wa taasisi zote zinawahudumia Walimu kufuatilia deni hilo lakini
wamepewa majibu yasiotekelezeka.
''Leo asilimia 70 ya walimu wamekata tamaa ya
kufundisha kutokana na serikali kushindwa kulipa deni lao na deni hili limekuwa
kubwa haijawai kutokea,huku walimu wakishangaa Rais John Magufuli
kununua ndege wakati anashindwa kuwalipa walimu”amesema Uluoch.
Amekichanganua madai hayo ya walimu Uluoch amesema
walimu wastaafu wanaidai serikali 556,048,000,0000 ,madeni ya mishahara
ya walimu waliopandishwa madaraja Januari hadi machi 2016 kwa walimu 85,945
wanaidai serikali jumla 301,374,321,000 huku akitahadharisha deni hilo
kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 25 kila mwezi ambapo ambapo amedai endapo
sekali isipolipa deni hilo mpaka Juni mwaka huu litaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mbali na madeni hayo yapo Madeni walimu 150, 000 ambao wanaidai mishahara
serikali jumla ya 180,000,000,0000,pia wapo walimu 36000 ambao hawajapanda
madaraja mwaka huu ambao walipaswa kupandishwa madaraja ndani ya mwaka
huu wa fedha ,hivyo wanaidai serikali 32,400,000,000.
Oluoch amesema licha madeni haya kuwasilisha kwa
serikali lakini wameshangaa serikali kuwalipa asilimia 10 tu ya madeni hayo ambayo ni bilion 124 tu.
Pamoja na hayo chama hicho kimeoneshwa mshangao wake
kwa serikali kusema walimu wa sanaa kutosha katika shule za sekondari nchîni
wakati bado kuna mahitaji makubwa ya walimu wa sanaa mashuleni.
''Kuna walimu 40000 wamemaliza vyuo wapo mtaani
wamemaliza vyuo hawana kazi na huku serikali ikisema walimu wa sanaa
wametosha,sio kweli bado kunamahitaji makubwa ya walimu wa sanaa wanaofiki elfu
50''amesema Uluouch.
Hata hvyo.chama hicho serikali kuwalipa walimu madai
yao na kuacha kujitetea haina fedha wakati serikali inanunua ndege.