TRA YAZIDI VUNJA REKODI YA MAKUSANYA YA MAPATO,YATOA TAARIFA YAKE KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetangaza kuvunja
rekodi ya ukosanyaji mapato katika mwaka wa fedha 2016-2017 katika kipindi cha
miezi sita toka Julai 2016 hadi Desemba 2016 mwaka jana baada kukusanya kodi ya jumla ya
shilingi trioni 7.27 ambapo ni sawa na asilimia 12.74 ya ongezeko la mapato
ikilinganishwa na Trion 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa
fedha 2015/2016.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu ya Mlipa kodi wa TRA,Richard Kayombo amesema ongezeko hilo la
mapato limetokana na Mamlaka hiyo kuziba
mianya ya ukwepaji kodi jambo lilochangia mapato hayo kuongezeka.
“Ongezeko hili limetokana na jitihada mbali mbali zilizofanywa na TRA
katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi,kuhimiza maadili mema kwa
watumishi,kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi,kushirikiana na vyombo vya
vingine vya dola na wananchi kuziba mianya upotevu wa mapato’amesema Kayombo.
Kayombo akichanganua mlinganisho wa ukusanyaji wa
mapato kwa mwaka wa fedha 2015-2016 na 2016/2017 amesema Julai 2015-2016 Mamlaka hiyo ilikusanya Bilioni 925.384.7
ambapo katika kipindi cha mwezi kama huo katika Mwaka 2016-2017 walifanikiwa
kukusanya Trioni 1.068.458.6 sawa ongezeko la asilimia 15.57.
Pia katika mwezi Agosti mwaka wa fedha 2015-2016
walikusanya Bilioni 923.316.9 ambapo pia
katika kipindi kama cha mwezi huo katika mwaka wa fedha 2016-2017 wamefanikiwa
kukusanya Trioni 1.154.222.5 ambapo ni sawa na asilimia 25.01.
Kayombo amesema Semptemba katika mwaka wa fedha
2015-2016 walikusanya trion 1.132.310.3 ambapo katika mwezi wa kama huo kwenye
mwaka wa fedha 2016-2017 wamefanikuwa kukusanya Trion1,378.048.9 ambapo sawa na
ongezeko la asilimia 21.70.
Octoba katika mwaka 2015-2016 walikusanya trion
1.037.179.8 na pia katika mwezi kama huo
mwaka 2016-2017 walikusanya trion 1.131.094.9 ambapo sawa na ongezeko la
asilimia 9.05.
Kayombo ameongeza kusema kuwa katika mwezi Novemba
mwaka 2015-2016 walikusanya trioni
1.027,393,6 na kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2016.2017 wamefaikiwa
kukusanya trioni 1,123,509.7 sawa na ongezeko la asilimia 9.30.
Hata hivyo pia katika mwezi Disemba katikamwaka
2015-2016 walikusanya Trion 1,403,189.8 huku pia katika kipindi kama hicho
katika mwaka 2016-2017 walifanikiwa kukusanya trion 1,414,921.8 sawa na
asilimia 0.84.
Pamoja na hayo Kayombo amewataka wafanyabiashara wote kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili
serikali ipate Mapato yake kwa wakati ambayo amedai yataweza kuwahudumia
Wananchi wake kikamilifu.
Pia amewahimzia
wafanyabiashara wote wenye madeni ya Nyumb a kujitokeza kuonana na
Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila
kuathiri biashara zao.