SERIKALI YA JPM YAKUBALI YAISHE KWA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA,SOMA HAPO KUJUA
Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na
Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia
kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.
Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na
wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,
George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa
mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa
tena.
''Hakukuwa na dhamira yeyote ya
kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza
kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili
tene upya swala hili" amesema
Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa
kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri
kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na
kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.
Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam
Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi
kulifanyioa kazi.