VIONGOZI WA UPINZANI WAZIDI KAMATWA NCHINI,SASA BALAA LAMUANGUKIA LOWASSA NAYE ATIWA MBARONI,SOMA HAPO KUJUA
EDWARD Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya
mkusanyiko usio halali, anaandika Charles William.
Lowassa
amekamatwa alasiri ya leo baada ya kukatiza kwa mguu katika eneo stendi ya
mabasi Geita, ambapo wananchi wengi walimzunguka wakimsalimia na kusababisha
msongamano mkubwa wa watu, kila mtu wakitaka kumsogelea.
Hata hivyo taarifa zaidi kutoka mkoani Geita
zimeeleza kwamba, mbali na Lowassa kukamatwa lakini pia baadhi ya waandishi wa
habari walipigwa na kukamatwa na askari waliofika eneo la tukio kumkamata
Lowassa.
“Askari walifika wakiwa katika magari matatu huku
wakiwa wamejihami kwa silaha za moto, wamewapiga waandishi wa habari na
kumkamata Lowassa ambapo wamempeleka Kituo Kikuu cha Polisi Geita,” kimeeleza
chanzo chetu.
Khamis Mgeja, mmoja kati ya watu waliokuwa
wameambatana na Lowassa katika msafara huo amesema, Lowassa alikuwa akielekea
sokoni kununua matunda na kwamba wanashangaa kwanini Polisi wamemkamata.
“Alikuwa anapita sokoni kununua matunda, watu
wakajazana kumsalimia na yeye kama mtu muungwana akawa akisalimiana nao, polisi
wakafika kumkamata na wamempeleka kituo kikuu cha polisi,” amesema kwa simu
Mgeja alipozungumza na MwanaHALISI Online.
Taarifa
zaidi kuhusu tukio hili zitakujia kwa kadri tutakavyokuwa tukipokea…